Ruka hadi maudhui
Biblia Takatifu
SW
Saidia mradi
Picha: Bintumani · Siera Leoni

Ayubu 25

Bintumani · Siera Leoni · Picha: Rokaso · CC BY-SA 4.0

1Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:

2“Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu; yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.

3Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?

4Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?

5Ikiwa hata mwezi sio mwangavu nazo nyota si safi machoni pake,

6sembuse mtu ambaye ni funza: mwanadamu ambaye ni buu tu!”

    Marejeo mtambuka kutoka OpenBible.info (CC BY 4.0).