Ruka hadi maudhui
Biblia Takatifu
SW
Saidia mradi
Picha: Mfereji wa Savuti · Botswana

Zaburi 87

Mfereji wa Savuti · Botswana · Picha: diego_cue · CC BY-SA 3.0

1Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

2Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.

3Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:

4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”

6Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”

7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

    Marejeo mtambuka kutoka OpenBible.info (CC BY 4.0).