Ruka hadi maudhui
Biblia Takatifu
SW
Saidia mradi
Picha: Funguvisiwa la Louisiade · Papua Guinea Mpya

Isaya 12

Funguvisiwa la Louisiade · Papua Guinea Mpya · Picha: Dayna Russell · Public domain

1Katika siku ile utasema: “Nitakusifu wewe, Ee Bwana. Ingawa ulinikasirikia, hasira yako imegeukia mbali nawe umenifariji.

2Hakika Mungu ni wokovu wangu; nitamtumaini wala sitaogopa. Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu; amekuwa wokovu wangu.”

3Kwa furaha mtachota maji kutoka visima vya wokovu.

4Katika siku hiyo mtasema: “Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake; julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya, tangazeni kuwa jina lake limetukuka.

5Mwimbieni Bwana, kwa kuwa ametenda mambo makuu, hili na lijulikane duniani kote.

6Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni, kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”

    Marejeo mtambuka kutoka OpenBible.info (CC BY 4.0).