Ruka hadi maudhui
Biblia Takatifu
SW
Saidia mradi
Picha: Kisiwa cha Wake · Marekani

Zaburi 70

Kisiwa cha Wake · Marekani · Picha: Alexander W. Riedel (U.S. Air Force) · Public domain

1Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi. Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie.

2Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu.

3Wale waniambiao, “Aha! Aha!” warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.

4Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu na atukuzwe!”

5Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Ee Mungu, unijie haraka. Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Ee Bwana, usikawie.

    Marejeo mtambuka kutoka OpenBible.info (CC BY 4.0).