Ruka hadi maudhui
Biblia Takatifu
SW
Saidia mradi
Picha: Machweo katika anga ya Hebroni · Palestina

Zaburi 129

Machweo katika anga ya Hebroni · Palestina · Picha: حسام أبوزينة · CC BY-SA 4.0

1Wimbo wa kwenda juu. Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:

2wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.

3Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.

4Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.

5Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.

6Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;

7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.

8Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”

    Marejeo mtambuka kutoka OpenBible.info (CC BY 4.0).