Ruka hadi maudhui
Biblia Takatifu
SW
Saidia mradi
Picha: Macheo katika matuta ya mchanga ya San Cosme y Damián · Paragwai

Zaburi 131

Macheo katika matuta ya mchanga ya San Cosme y Damián · Paragwai · Picha: Krizlez · CC BY-SA 4.0

1Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.

2Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.

3Ee Israeli, mtumaini Bwana tangu sasa na hata milele.

    Marejeo mtambuka kutoka OpenBible.info (CC BY 4.0).