Ruka hadi maudhui
Biblia Takatifu
SW
Saidia mradi
Picha: Machweo katika Jangwa la Kalahari · Namibia

Zaburi 67

Machweo katika Jangwa la Kalahari · Namibia · Picha: Giles Laurent · CC BY-SA 4.0

1Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo. Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake,

2ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote.

3Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

4Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia.

5Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

6Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

7Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

    Marejeo mtambuka kutoka OpenBible.info (CC BY 4.0).